Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa Rais kuburuzwa kortini ubadhilifu fedha za umma

Alibongo Copie 1 (600 X 383) Watoto wa Rais kuburuzwa kortini ubadhilifu fedha za umma

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wanne wa Rais wa zamani wa Gabon, Omar Bongo wamefunguliwa mashitaka Nchini Ufaransa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya mali za makampuni na rushwa.

Watoto hao Grace, Betty, Arthur na Hermine Bongo, wote wakiwa na zaidi ya miaka 50 walifunguliwa mashitaka hayo baada ya uchunguzi.

Wapelelezi wanaamini familia na jamaa wa hayati Bongo akiwemo Omar, Ali ambaye ndiye Rais wa Gabon, na Pascaline walinufaika kwa kujua kutokana kumiliki mali isiyohamishika iliyopatikana kwa njia ya udanganyifu yenye thamani ya Dola milioni 93.

Watoto wanne waliofunguliwa mashitaka wameka kuhusika na ulaghai unaotajwa dhidi yao.

Wamesema kuwa walipokea mali hizo zilizopo Jijini Paris kama zawadi kutoka kwa baba yao kati ya mwaka 1995 na 2004.

Omar Bongo alitawala Gabon kuanzia mwaka 1967 hadi alipofariki 2009 alipofariki na nafasi yake kuchukuliwa na mwakane, Ali.

Inadaiwa Omar Bongo alikuwa na watoto 54 ambao nao wengi wao wanaweza kukabiliwa na makosa mbalimbali.

Alipotafutwa Msemaji wa Ikulu ya Gabon, Jessye Ella Ekogha alikataa kutoa neno lolote kuhusu suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live