Afisa wa afya katika Jimbo la Kwilu, takriban kilomita 680, mashariki mwa Mji Mkuu wa DRC, Kinshasa alimeviambia vyombo vya habari kuwa karibu watoto 7,000 waliambukizwa na kwa sasa wanatibiwa.
Dalili ni pamoja na homa kali na kuhara. Mlipuko huo ulianza Agosti mwaka huu. Novemba 7 mwaka jana, sampuli zilifika katika Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Biolojia, mjini Kinshasa ili kubaini chanzo cha ugonjwa huo.
Mgomo wa wafanyakazi wa matibabu katika Mkoa wa Kwilu ulicheleweshwa tahadhari ya mapema
Watoto 286 wenye umri wa kati ya mwaka 0 na 5 walifariki katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na ugonjwa ambao haukujulikana asili yake,
Mkuu wa kitengo cha afya cha jimbo la Kwilu Jean Pierre Baseke alithibitisha haya kwenye redio ya umoja wa mataifa katika jahmuri ya kidemokrasia ya Congo maarufu radio okapi.
Alibainisha kuwa tangu mwishoni mwa Agosti ugonjwa huu ulipotokea, kumekuwa na zaidi ya maambukizi 7000 sasa ikiwa ni pamoja na vifo 286. Dalili ni pamoja na homa na maumivu ya tumbo, kutapika na upungufu wa damu
Daktari Jean Pierre Basele anahisi kwamba ni janga jipya, kwa sasa sampuli zimefikishwa mji mkuu Kinshasa kwenye taasisi ya serkali inaoyochunguza sampuli tangu tarehe saba mwezi huu , na sasa wanaendelea kusubiri matokeo.
" Tulianza na visa zaidi ya elfu tano lakini kwa sasa tumekuwa na visa zaidi ya elfu saba tangu tarehe nane ya mwezi huu na watoto mia mbili na thamanini na sita wameshafariki.
Takwimu ni hizo hizo tu kwasasa kwabababu serkali ya jimbo ilitoa pesa na tumeeanza kutoa matibabu kwa watoto, kwa sasa tumengudua kama ni malaria lakini tukilinganisha na miaka iliyopita, kesi zinaongezeka kwa mara tano kwa hiyo tunaona ya kwamba limekuwa janga linigine jipya" Alisema Dkt. Basele.
Kituo cha afya cha Mukedi ambako kesi ya kwanza iliripotiwa tangu tarehe 15 Agosti , wakati maafisa wa afya walipokuwa katika mgomo na hivyo ulichelewesha viongozi wa ngazi ya juu kufatilia haraka ,na kwa sasa karibu watoto mia tatu wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi mitatu na takribani watoto 7000 wameugua.
Shirika la raia jimboni kwilu linalaumu serkali ya Congo kuchelewesha jibu lake kila mara kukiwa mlipuko wa janga .
Kwa mujibu wa placide Mukwa kiongozi wa shirika la raia jilmboni kwilu, haiwezi heleweka kuona zaidi ya watoto mia mbili wamefariki kwa kipindi cha miezi mitatu katika jimbo hilo ambalo linapakana na mji mkuu kinshasa na ni siku moja tu kwa njia ya gari ndo maafisa wa afya wanaweza kufika huko na kupata suluhisho .
Shirika la raia linataka idara ya serikali inayochunguza sampuli kuharakisha utafiti ili wafahamu haraka ugonjwa gani huo unaosababishavifo vya watoto.