Mapacha tisa pekee duniani - watoto waliozaliwa kwa wakati mmoja - wamerejea salama nchini Mali, nchi yao.
Wazazi na watoto wao tisa walifika katika uwanja wa ndege katika mji mkuu, Bamako, Jumanne na kukaribishwa na Waziri wa Afya Diéminatou Sangaré.
Walikuwa wakiishi katika eneo la matibabu huko Casablanca tangu waondoke katika zahanati ya Ain Borja ambapo watoto hao walizaliwa tarehe 4 Mei 2021.
Watoto hao walivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi waliozaliwa wakati mmoja kuishi.
Watoto hao - wasichana watano na wavulana wanne - walitungwa mimba kwa kutumia matibabu ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi (IVF) na walizaliwa kwa kupitia upasuaji.