Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto milioni 1 hatarini kukosa shule kutokana na usalama

Nigeriaaa.png Watoto milioni 1 hatarini kukosa shule kutokana na usalama

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: Jamii Forums

Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Watoto (UNICEF) limesema Watoto Milioni 1 huenda wasiende Shule kutokana na matukio ya utekaji nyara yanayolenga Wanafunzi

Zaidi ya Wanafunzi 1,000 wametekwa nyara na magenge ya uhalifu katika Majimbo kadhaa #Nigeria tangu Desemba 2020, huku mamia bado wakiendelea kushikiliwa.

Kwa mujibu wa UNICEF, mashambulizi 20 yametokea Shuleni mwaka 2021 ambapo Wanafunzi 1,400 walitekwa na 16 kupoteza maisha. Wengi wao huachiwa baada ya wahalifu kulipwa fedha.

Kufuatia matukio hayo yakiualifu ni dhahiri kuwa maisha ya Watoto mashuleni ni hatari na pia kupelekea watoto wengi kupata hofu ya kwenda shule.

Chanzo: Jamii Forums