Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 8 kati ya 10 wanatatizika kusoma umri wa miaka 10 Afrika Kusini

Watoto 8 Kati Ya 10 Wanatatizika Kusoma Umri Wa Miaka 10 Afrika Kusini Watoto 8 kati ya 10 wanatatizika kusoma umri wa miaka 10 Afrika Kusini

Wed, 17 May 2023 Chanzo: Bbc

Watoto nane kati ya 10 wa shule nchini Afrika Kusini wanatatizika kusoma kufikia umri wa miaka kumi, utafiti wa kimataifa umegundua.

Afrika Kusini iliorodheshwa ya mwisho kati ya nchi 57 zilizofanyiwa tathmini katika Utafiti wa Kimataifa wa Kusoma na Kuandika, ambao ulijaribu uwezo wa kusoma wa wanafunzi 400,000 duniani kote mwaka wa 2021.

Kiwango cha kutojua kusoma na kuandika miongoni mwa watoto wa Afrika Kusini kilipanda kutoka 78% mwaka 2016 hadi 81%.

Waziri wa elimu nchini humo alilaumu matokeo hayo kwa kufungwa kwa shule wakati wa janga la Covid-19.

Akielezea matokeo hayo kuwa "ya chini na ya kukatisha tamaa", Angie Motshekga pia alisema mfumo wa elimu nchini unakabiliwa na changamoto kubwa za kihistoria, ikiwa ni pamoja na umaskini, ukosefu wa usawa na miundombinu duni.

Katika shule nyingi za msingi "maelekezo ya kusoma mara nyingi huzingatia tu utendaji wa kuzungumza, huku yakipuuza ufahamu wa kusoma na kuleta maana ya maneno yaliyoandikwa", aliongeza.

Utafiti ulionyesha kuwa 81% ya watoto wa Afrika Kusini hawakuweza kusoma kwa ufahamu katika lugha yoyote kati ya 11 rasmi nchini humo.

Pamoja na Morocco na Misri, Afrika Kusini ilikuwa mojawapo ya nchi tatu za Afrika ambazo zilishiriki katika tathmini za kufuatilia mienendo ya kusoma na kuandika na ufahamu wa kusoma wa watoto wa miaka tisa na 10.

Kulingana na majaribio yanayofanywa kila baada ya miaka mitano mwishoni mwa mwaka wa shule, utafiti mpya unaweka nchi katika jedwali la ligi ya kimataifa ya elimu.

Singapore ilijihakikishia nafasi ya kwanza katika viwango hivyo ikiwa na wastani wa alama 587, huku Afrika Kusini ikishika nafasi ya mwisho kwa pointi 288 - chini ya Misri iliokuwa na alama 378. Alama hizo zimewekwa dhidi ya wastani wa alama 500 za kimataifa.

Utafiti pia ulionyesha kuwa kwa ujumla, wasichana walikuwa mbele ya wavulana katika ufahamu wao wa kusoma katika karibu nchi zote zilizotathminiwa, hatahivyo pengo la kijinsia limepungua katika duru ya hivi karibuni ya majaribio.

Mapambano ya Afrika Kusini na mfumo wake wa elimu ni ya muda mrefu, na ukosefu mkubwa wa usawa kati ya wanafunzi weusi na weupe ni matokeo ya kutengwa kwa watoto chini ya ubaguzi wa rangi.

Elimu ni moja ya gharama kubwa zaidi za bajeti ya serikali, ambayo huenda ikakatizwa tamaa na matokeo duni katika masomo kama haya.

Ukosefu wa nyenzo zinazofaa za kusoma na miundombinu duni shuleni, kama vile vyoo, kumechangia tatizo hilo.

Chanzo: Bbc