Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watengeneza maudhui ya Tiktok Kenya washtakiwa

Watengeneza Maudhui YaTiktok Washtakiw Watengeneza maudhui yaTiktok Kenya washtakiwa

Fri, 10 May 2024 Chanzo: Bbc

Watengeneza maudhui wanne wa TikTok waliokamatwa kwa kurekodi video ya maigizo ya wizi uliofanywa nje ya kituo cha polisi katika pwani ya Kenya wameshtakiwa kwa kuchapisha habari za uongo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Watengenezaji maudhui hao akiwemo mvulana wa umri wa miaka 17, walikamatwa Jumatano katika kaunti ya Kilifi baada ya video hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo ya kuigiza, mwanamume mmoja anatoka katika kituo cha polisi cha Kilifi na kunyang'anywa begi lake na watu wengine wawili waliokuwa kwenye pikipiki inayomsubiri, almaarufu boda boda.

Polisi walisema watu hao walikamatwa baadaye baada ya kutambuliwa kupitia kamera ya CCTV katika kituo hicho.

Washukiwa hao walichapisha video hiyo kwenye mtandao wa TikTok ikiwa na nukuu "majambazi nje ya kituo cha polisi cha Kilifi", ambayo walijua ni ya uwongo, mahakama ilisikiza kesi hiyo Alhamisi.

Wanne hao walikanusha mashtaka na walipewa dhamana ya $1,500 (£1,200), tovuti ya habari ya Nation iliripoti.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 30 Julai.

Chanzo: Bbc