Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya eneo la Kasarani jijini Nairobi – Kenya, Anthony Mbogo amethibitisha kutokea kwa tukio la kuporomoja kwa Jengo la Ghorofa sabana kusababisha vifo vya watu watatu huku sita wakiokolewa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mbogo ameyasema hayo hii leo Novemba 16, 2022 na kusema bado wanaendelea kukusanya taarifa za utambulisho wa watu wanaohofiwa kunaswa kwenye kifusi na kusema wafanyakazi wa ujenzi katika eneo hilo walianza kuona nyufa majira ya asubuhi ya kutoa taarifa.
Mara baada ya tarifa hizo, inasemekana Msimamizi wa Ujenzi alisisitiza watu kuendelea na kazi akiwataka kupuuza habari hizo kwa kusema jengo hilo lilikuwa salama hali abayo ilikuwa ni tofauti na watu wanne waliokolewa na wanane walinasa ndani huku uokoaji ukiendelea.
Hili ni jengo la pili kuporomoka jijini Nairobi ndani ya wiki moja, ambapo Jumatatu ya Novemba 7, jengo la orofa nane ambalo pia lilikuwa likijengwa liliporomoka huko Tassia, Embakasi. Justus Mutisya, 38, ndiye pekee aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.