Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wawili wafa ajalini Zambia

Ajali Zambia2162 Watanzania wawili wafa ajalini Zambia

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wawili wa Tanzania, watatu wa Zambia na mmoja wa Kenya wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Serenje nchini Zambia, huku watu wengine 42 wakijeruhiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 27 Disemba 2023 na Afisa Mahusiano kwa Umma wa Jeshi la Polisi Zambia, Rae Hamoonga, ajali hiyo ilitokea juzi Jumanne, ikihusisha basi la abiria la Mkombe Luxury, lililokuwa linatokea jijini Johannesburg Afrika Kusini, kuja Dar es Salaam Tanzania kupitia Zambia, pamoja na lori la mizigo.

Ajali hiyo ilitokea mchana wa tarehe 26 Disemba 2023, baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, lililokuwa linatokea Tanzania kwenda Zambia.

Hamoonga ametaja majina ya watu waliopoteza maisha kuwa ni, Davies Kolala (Mzambia), aliyekuwa dereva wa lori la mizigo, Rashid Athumani (Mtanzania), Chibala Abdnegal (Mzambia), Oscar Mwamulima (Mzambia), Ramadhan Abdallah (Mtanzania) na Eunice Jose (Mkenya).

Watoto nane ni miongoni mwa majeruhi 42 wa ajali hiyo, Watanzania waliojeruhiwa walikuwa 14, Wakenya nane, Wazambia 19 na mmo kutoka Uganda.

Taarifa ya Hamoonga imesema majeruhi wanaendelea kutibiwa katika hospitali nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live