Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wateuliwa Baraza la Biashara EAC

90ad60c9285a50af0819358eadead6aa.jpeg Watanzania wateuliwa Baraza la Biashara EAC

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA la Biashara ya Afrika Mashariki (EABC) limefanya uteuzi wa wajumbe wanne kupitia kikao cha Kamati Kuu ya Baraza hilo, wakiwamo Watanzania.

Wajumbe walioingia katika baraza hilo ni Paul Koyi ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Kilimo, Viwanda na Biashara nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo baada ya kumalizika kwa kikao hicho ilieleza kuwa, maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na uteuzi wa wajumbe hao.

Wajumbe wengi walioteuliwa ni Paul Makanza ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Jaqueline Mkindi ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kilimo cha Mboga za Majani Tanzania (TAHA).

Mjumbe mwingine aliyeteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo ni Ali Suleiman Amour, ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Kitaifa ya Zanzibar (ZNCC).

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 1997 likilenga kuimarisha biashara katika sekta binafsi na kukuza uhusiano baina ya mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.habarileo.co.tz