Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umewataka Watanzania waishio nchini humo kuchukua tahadhari baada ya kiongozi wa chama cha Marxist Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema nchini humo kuitisha maandamano ya amani ya kitaifa kushinikiza Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ajiuzulu.
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umewataka Watanzania waishio nchini humo kuchukua tahadhari baada ya kiongozi wa chama cha Marxist Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema nchini humo kuitisha maandamano ya amani ya kitaifa kushinikiza Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ajiuzulu. Taarifa iliyotolewa na Ubalozi imewataka Watanzania kuwa watulivu na kujiepusha na kujihusisha kwa namna moja ama nyingine katika matukio ya maandamano na mgomo wa kitaifa.