Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wapasua soko la soya China

Da4ffa42db3d28eb49cb1c8cb9055fed Watanzania wapasua soko la soya China

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI 49 za Kitanzania zimeidhinishwa na Mamlaka ya Forodha China kuuza maharage ya soya kutoka nchini kuuzwa katika nchi hiyo.

Taarifa hiyo ilitolewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, alipofanya mawasiliano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa njia ya mtandao.

Alisema mafanikio ya hatua hizo ni matokeo ya mkataba uliosainiwa baina ya Tanzania na China Oktoba mwaka jana ambao nchi hiyo iliruhusu kusafirisha bidhaa hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema hayo ni mafanikio ya kazi kubwa inayoendelea kufanywa na mamlaka kuunganisha wafanyabiashara wa wa nchini na nchi mbalimbali.

Alisema wamekuwa na mikutano ya kibiashara kwa njia ya mtandao tangu Julai mwaka jana kuwaunganisha wafanyabiashara wa nchi za Mashariki ya Kati na Asia ikiwemo Malaysia, Indonesia na Ufilipino, Saudi Arabia, Kuwait, Qatar na Oman kwa kushirikiana na mabalozi.

Aliongeza kuwa, China ni soko kubwa na uhitaji wao ni tani milioni 103 kati ya tani milioni 88 zinaagizwa kutoka mataifa mbalimbali.

Alisema Tanzania imefanikiwa kusafirisha tani 142 za maharage ya soya Machi 12 mwaka huu na inatarajia kusafirisha zaidi tani 13,000.

Rutageruka alitoa mwito kwa wakulima wa Tanzania waitumie Wizara ya Kilimo kuwasaidia katika uwezo wa kuzalisha maharage ya aina ya soya ili wakidhi viwango vinavyohitajika na soko hilo la China.

Chanzo: www.habarileo.co.tz