Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wanadaiwa kuwa na mahusiano na kundi la Wagner washtakiwa Ghana

Watano Wanadaiwa Kuwa Na Mahusiano Na Kundi La Wagner Washtakiwa Ghana Watano wanadaiwa kuwa na mahusiano na kundi la Wagner washtakiwa Ghana

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Ghana imewashtaki watu watano mahakamani kwa kujaribu kuanzisha kundi linaloshukiwa kuwa la Wagner nchini humo.

Washukiwa hao walikamatwa mwezi uliopita katika mji wa kusini wa Takoradi.

Hatua hiyo inakuja wakati Urusi inaonekana kupanua nyanja yake ya ushawishi katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kundi la vijana hao wakiwemo wanafunzi walikuwa wameandaa hafla ya kuzindua kikundi cha kijeshi mwezi uliopita walipokamatwa na polisi huko Takoradi.

Wanaodaiwa kufadhiliwa na watu binafsi nje ya nchi, baadhi yao walivalia mashati yenye chapa ya mamluki ya Wagner na kupandisha bendera za nchi tofauti, ikiwamo Urusi.

Mwanamke mmoja kutoka eneo la Ramatu Ibrahim aliiambia BBC kwamba washukiwa hao walikuwa wamepanga kile walichokitaja kuwa maandamano ya uhuru wa Wagner.

Polisi nchini Ghana bado hawajatoa taarifa rasmi za kukamatwa kwa kwao.

Urusi, kupitia kundi lake la mamluki, inapanua nyanja yake ya ushawishi barani Afrika, ikiwa na uwepo mzuri katika nchi ya Afrika Magharibi ya Sahel ya Mali pamoja na Libya, Sudan, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Chanzo: Bbc