Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano familia moja wachinjwa, nyumba zateketezwa

PANGA Ed Mauaji

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Zaidi ya watu watano wa familia moja nchini Kenya, wamekutwa wamechinjwa na watu wanaoaminika kuwa ni wanamgambo wa kundi la uasi la Al – Shabab.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Taarifa vya idara ya Polisi jijini Nairobi, vimesema tukio hilo limetokea katika eneo la Salama, lililopo Kibaoni kaunti ya Lamu na kwamba hakuna mali nyingine iliyoharibiwa wala mtu aliyejeruhiwa.

Inaarifiwa kuwa, magaidi hao walivamia Kijiji cha Salama usiku wa kuamkia leo Juni 25, 2023 na kuwatoa watu hao ndani ya nyumba zao na kuwachinjaa kisha kuteketeza moto nyumba mbili.

Hata hivyo, bado haijafahamika mara moja nia ya watu hao, ambao hawakuacha ujumbe wala kusema lolote, huku vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya vikisema, vimeimarisha ulinzi na msako wa kuwatafuta wahusika unaendelea.

Chanzo: Mwanaspoti