Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi watanda juu ya mapigano ya Sudan, kufika Sudan Kusini

Wasiwasi Watanda Juu Ya Mapigano Ya Sudan, Kufika Sudan Kusini Wasiwasi watanda juu ya mapigano ya Sudan, kufika Sudan Kusini

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mjumbe wa kikanda wa Umoja wa Mataifa alielezea wasiwasi wake Jumatatu kwamba mapigano kati ya majeshi ya majenerali wawili wanaowania mamlaka Sudan, yanakaribia mpaka wa nchi hiyo na Sudan Kusini, na jimbo lenye mgogoro la Abyei.

Mgogoro uliozuka mwezi Aprili kati ya wanajeshi watiifu kwa mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na kikosi cha dharura (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, una matokeo makubwa ya kibinadamu, kiusalama, kiuchumi na kisiasa ambayo ni masuala yenye kuzua wasiwasi mkubwa kwa utawala wa kisiasa wa Wasudan Kusini, alisema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Pembe ya Afrika, Hanna Tetteh.

Pamoja na mashambulizi yake ya kijeshi huko Kordofan Magharibi na kutwaa uwanja wa ndege wa Belila na visima vya mafuta, RSF inakaribia Abyei, ikidhibiti sehemu za mpaka na Sudan Kusini, Tetteh alisema wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Chanzo: Bbc