Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi watanda baada ya pipa linalotiliwa shaka kupatikana pwani ya Somalia

C801BF4E 9272 4C5B 9D74 C43DEF996C1C.jpeg Wasiwasi watanda baada ya pipa linalotiliwa shaka kupatikana pwani ya Somalia

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Somalia wameonywa kutokaribia pipa lililozibwa ambalo limesombwa na maji kwenye ufuo wa Puntland, huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda lina taka za sumu.

Pipa hilo la bluu lililofungwa limeunganishwa na kamba na maafisa wanashuku kuwa lilitupwa baharini na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa gazeti la The East African, pipa hilo lilipatikana katika eneo la Mudug katikati mwa Somalia, ambako fukwe kwa ujumla ni safi.

Pipa hilo lilisombwa wiki hii huko Ilfohshe, karibu na mji wa Jariban, yapata kilomita 900 kaskazini-mashariki mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Hii si mara ya kwanza kwa jamii za pwani kuona mapipa ya ajabu yanayoelea kwenye maji yao.

Mwaka 2004, Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) ulipata mapipa ya nyenzo zisizojulikana kwenye pwani karibu na Puntland. Makampuni yasiyojulikana kutoka Ulaya awali yalilaumiwa kwa kutumia maji ya Somalia yenye ulinzi duni kutupa taka zenye sumu.

Hakujawa na tathmini sahihi ya ukubwa wa utupaji taka huo, lakini baadhi ya makadirio yanaonyesha kuwa hadi tani milioni 35 za taka zimetupwa kinyume cha sheria katika maji ya Somalia, ikiwa ni pamoja na taka za hospitali, viwanda na hata taka hatari za nyuklia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live