Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi watanda SADC, M23 wakirejesha mapigano

Kiongozi Wa Upinzani Ufaransa Akemea Kundi La M23 Wasiwasi watanda SADC, M23 wakirejesha mapigano

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakuu wa nchi mbalimbali za ukanda wa kusini mwa Afrika wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakisema kukwa mashambulizi ya waasi wa M23 ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano."

Viongozi hao wameonesha wasiwasi wao huo wakati wa mkutano wa kilele uliofanyika jana Jumamosi huko Luanda, mji mkuu wa Angola.

Kwa mujibu wa taarifa ya kikao hicho cha dharura cha wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola, viongozi hao wameonesha wasiwasi wao mkubwa kuktokana na kuzorota usalama na hali ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Viongozi hao pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu ripoti zinazoonesha kuanza tena mashambulio ya waas wa M23 na kuteka na kuyakalia kwa nguvu maeneo mapya nchini humo.

Nchi 12 wanachama wa SADC zimehudhuria mkutano huo wa jana wa mjini Luanda. Marais waliohudhuria mkutano huo ni wa Tanzania, Angola, DRC, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live