Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi nchini Gabon kuhusu nia ya viongozi wa mapinduzi

Wasiwasi Nchini Gabon Kuhusu Nia Ya Viongozi Wa Mapinduzi Wasiwasi nchini Gabon kuhusu nia ya viongozi wa mapinduzi

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Muungano wa upinzani nchini Gabon umelishutumu jeshi kwa kutoonyesha dalili zozote kwamba wanapanga kurudisha madaraka kwa serikali ya kiraia baada ya kumutimua madarakani Rais wa zamani Ali Bongo.

Msemaji wa muungano huo, Alexandra Pangha, aliambia kipindi cha Newsday cha BBC kuwa itakuwa upuuzi kwa wafuasi hao kumuapisha rais siku ya Jumatatu kabla ya taasisi walizozivunja.

Alikosoa kusita kwao kufanya mazungumzo na chama alichosema kilishinda uchaguzi wa urais wa Jumamosi iliyopita.

“Kufikia leo tumekuwa tukisubiri mwaliko kutoka kwa wanajeshi ili watueleze mpango wao ni upi,” Bi Pangha alisema na kuongeza kuwa haamini kwamba nasaba ya Bongo imeondoka mamlakani.

Alidai, bila kutoa ushahidi, kwamba kiongozi wa mapinduzi, Jenerali Brice Oligui Nguema, alikuwa akiungwa mkono na wanafamilia wengine.

Chanzo: Bbc