Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiomuamini Mungu wajitolea kumlipia mchekeshaji Jemutai kodi ya nyumba

925f7b7d0fc02db0 Wasiomuamini Mungu wajitolea kumlipia mchekeshaji Jemutai kodi ya nyumba

Mon, 3 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Rais wa Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Nchini (AKS) Harrison Mumia alimuomba Jemutai kuwasiliana nao ili apate usaidizi

- Chama hicho pia kilisema akina mama wasimbe ndio wanaathiriwa pakubwa na kuomba serikali kuwatafutia hazina

- Pia waliomba Bodi ya Kukagua Filamu Nchini (KFCB) na kanisa kuwasaidia wasanii wanaohangaika

Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Nchini (AKS) kimejitolea kumsaidia mvunja mbavu Stella Jemutai kulipa kodi kufuatia shutuma dhidi ya baba ya wanao Professor Hamo.

Katika taarifa, rais wa chama hicho Harrison Mumia alimuomba Jemutai kuwasiliana nao ili apate usaidizi

Mumia alisema maisha ya wasanii wengi yameathiriwa na janga huku akimtaja aliyekuwa muigizaji wa Tahidi High, Omosh kama mfano wa wale wanaohitaji msaada.

Chama hicho pia kilisema akina mama wasimbe ndio wanaathiriwa pakubwa na kuomba serikali kuwatafutia hazina.

"Tunaomba seriklai kutenga kando hazina ya akina mama wasimbe nchini Kenya. pesa hizi zinatakiwa kuwasaidia akina mama wanaothrika kiafya, kulea watoto na magonjwa," ilisoma taarifa hiyo.

Mumia pia aliwaomba Bodi ya Kukagua Filamu Nchini (KFCB) na kanisa kuwasaidia wasanii wanaohangaika.

Awali, Hamo alikuwa ameshikilia kwamba hajawakimbia watoto wake kama alivyodai Jemutai akisisitiza amekuwa akiwashughulikia.

Hamo alisema matusi ambayo yamekuwa kwenye mtandao tangu Jemtai afichue hayo yanawaathiri wanawe shuleni pakubwa.

Na hivyo hatajihusisha na majibizano yoyote ili kuwalinda wanawe.

Hata hivyo, Jemutai amefichua kuwa mara ya mwisho mchekeshaji huyo kukutana na watoto wake ilikuwa Oktoba 2020 kabla ya kuondoka nyumbani kwao.

Jemutai alisema tangu siku hiyo, ameonekana nyumbani kwake mara nne pekee akiwasili usiku wa manane akiwa mlevi chakari.

Kisha alimuomba kukubali ameshindwa majukumu yake kama baba na kuwa tayari kujirekebisha.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke