Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiojulikana waacha jeneza nje ya nyumba lenye misalaba mitatu

Jeneza.jpeg Wasiojulikana waacha jeneza nje ya nyumba lenye misalaba mitatu

Wed, 19 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Familia katika kijiji cha Ebunyang’anyi kata ya Bunyala, Kakamega nchini Kenya imepatwa na mshtuko baada ya kuamka na kukuta jeneza lililokuwa na misalaba mitatu likiwa limewekwa mlangoni  nje ya mlango wa nyumba ya Peter Wekondi, mzee mkongwe ambaye pia ni mgonjwa.Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho cha kushangaza, Janepher Masika amesema kuwa jeneza hilo lilikuwa limefungwa kwenye kitambaa cheupe huku nzi wakiwa wamejaa juu yake.

 “Nilipokuwa nikienda shambani niliona jeneza nje ya nyumba ya majirani zangu na nikawaamsha kuwaarifu. Nilishtuka kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho maishani,” Masika.

Kwa muda mfupi, tukio hilo lilikuwa limevuta umati mkubwa uliokusanyika katika nyumba hiyo kushuhudia kisa hicho kilichowaacha midomo wazi.

Baada ya kufungua jeneza hilo wenyeji hao waliachwa na mshtuko baada ya kupata mchanga na vifaa vingine visivyojulikana. Baadhi yao walikihusisha kisa hicho na ushirikina ambao walisema huenda mhusika alichukua hatua hiyo kutokana na wivu.

Jotham Makokha, mzee wa ‘nyumba kumi’ alitoa wito kwa wenyeji kupendana na kuishi kwa amani na uwiano.

DIAMOND AWAVAA FORBES UTAJIRI, DROGBA, DON JAZZY WAKUBALI NI TAJIRI AFRIKA

Chanzo: millardayo.com