Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washukiwa wakamatwa wakihusishwa na genge la ubakaji Kenya

Washukiwa Wakamatwa Wakihusishwa Na Genge La Ubakaji Kenya Washukiwa wakamatwa wakihusishwa na genge la ubakaji Kenya

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Kenya wamewatia mbaroni washukiwa saba kuhusiana na kujihusisha na genge la kumbaka mwanamke katika kaunti ya Bomet magharibi.

Tukio hilo, lililonaswa kwenye video ya mtandaoni, lilitokea katika kijiji cha Chebanyi Desemba mwaka jana, polisi walisema. Kipande cha video kinachosambaa kama "sigor boys" kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, inawaonesha wanaume kadhaa kwenye chumba chenye mwanga hafifu wakipokezana kumnyanyasa kingono mwanamke, ambaye anasikika akipiga kelele.

Video hiyo imeshangaza nchi, huku wengi wakitaka haki itendeke kwa mwanamke huyo ambaye hajatambulika.

Polisi walisema katika taarifa siku ya Alhamisi waliwakamata washukiwa hao kufuatia operesheni katika eneo hilo.

Washukiwa wawili walitambuliwa na polisi wanasema wanawasaka watu wengine.

Polisi walisema watawafikisha washukiwa hao mahakamani na kutuma maombi ya kuwashikilia kwa muda mrefu ili kukamilisha uchunguzi.

Chanzo: Bbc