Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washukiwa Wanne wa Ujambazi Wauawa

0fgjhs5c4p3dd27tg Washukiwa Wanne wa Ujambazi Wauawa

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu wanne wanaoshukiwa kuwa majambazi walipigwa hadi kufa eneo la Liwatoni na wakaazi wa Mombasa mnamo Jumatano, Machi 24, baada ya kunaswa wakijaribu kutekeleza uhalifu.

Kulingana na ripoti ya Citizen Digital, wapangaji wa Amani Estate waliwashambulia wanne hao kwa silaha butu huku wakifukuzana nao katika makazi hayo.

"Leo wacha tuwaangamize hawa majangili ndio iwe funzo kwa wengine wote," wakaazi walisikika wakisema huku wakiwavamia.

Polisi huko Mombasa walithibitisha kuwa wanne hao walifumaniwa baada ya kuvunja nyumba za baadhi ya wakazi a kujaribu kuwapora mali yao.

Maafisa hao waliongeza kuwa genge hilo lilipenyeza hadi katika eneo hilo kwa kutumia pikipiki baada ya kukwepa vizuizi vya polisi.

Majambazi hao waliokuwa wamejihami kwa silaha walimdunga kisu mlinzi ambaye alikimbizwa hospitalini baada ya kupata majeraha mabaya tumboni.

Mlinzi wa pili aliyeshuhudia kisa hicho alipiga kamsa na kuwaamsha wenyeji ambao walichukua hatua mikononi mwao na kuwaadhibu majambazi hao.

Polisi walipata visu na mapanga ambayo walikuwa wakitumia kuwatishia wakaazi.

Miili ya majambazi hao wanne ilipelekwa katika makafani ya Mombasa General.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke