Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washirika wa Raila katika eneo la Kibra wamtoroka na kuhamia kambi ya Ruto

E48be26b6f7f7775 Washirika wa Raila katika eneo la Kibra wamtoroka na kuhamia kambi ya Ruto

Fri, 11 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Uamuzi huo ulitangazwa na Katibu Mkuu wa UDA Veronica Maina siku ya Alhamisi, Juni 10

- Picha za maafisa hao wa ODM wakipokelewa na Maina zilitundikwa kwenye kurasa za mtandao jamii za UDA

- Taarifa hiyo ilizua hisia mseto miongoni mwa Wakenya kwani eneo la Kibra ni ngome la kisiasa la kiongozi wa ODM Raila

Kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga amepata pigo kubwa baada ya wanachama wa chama hicho eneo bunge la Kibra, kaunti ya Nairobi kuhamia chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachohusiana na Naibu Rais William Ruto.

Uamuzi huo ulitangazwa na Katibu Mkuu wa UDA Veronica Maina siku ya Alhamisi, Juni 10.

Picha za maafisa hao wa ODM wakipokelewa na Maina zilitundikwa kwenye kurasa za mtandao jamii za UDA.

Washirika hao wa zamani wa Raila Odinga wanaripotiwa kukumbatia vuguvugu la 'hastla' Uchaguzi Mkuu wa 2022 unapokaribia.

"Katibu Mkuu Veronica Maina anawapokea wanachama wa ODM kutoka eneo bunge la Kibra ambao walihamia UDA. Wanaunga mkono vuguvugu la UDA la hustlers' ambalo wanasema linaafikiana na wakazi wa Kibra," ilisema chama hicho kwenye taarifa.



Taarifa hiyo ilizua hisia mseto miongoni mwa Wakenya kwani eneo la Kibra ni ngome la kisiasa la kiongozi wa ODM Raila.

Hanningtone Muchera alisema: "Msimu wa kuhama na kubadilisha wimbo na viti umefika. Tunawatakia kila la heri msimu huu."

Mugambi Amathi: "@UDAKenya inashinda nyumbani na nje."

@Paperboyrocks : "Wanaonekana wamepotea si vyema."

Kugura kwa wanachama wa ODM na kuhamia UDA kunakujia kufuatia kujiuzulu kwa katibu wa maandalizi James Agumba Sigar.

Sigar aligura chama hicho kabla ya uchaguzi mdogo wa Kibra 2019 ambapo mgombea wa ODM Imran Okoth aliibuka mshindi na kufuata nyayo za marehemu kaka yake Ken Okoth.

Kujiuzulu kwake ni baada ya msaidizi wa zamani wa Raila, Eliud Owalo kutema chama hicho cha upinzani na kujiunga na chama cha Musalia Mudavadi, Amani National Congress.

Owalo ambaye aliwania kiti cha ubunge cha Kibra alipoteza lakini baadaye alijiunga na kambi ya Ruto.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke