Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washirika wa Naibu Rais Ruto watishia kutaja mali za Rais Uhuru

Cb58c947b8a48f60 Washirika wa Naibu Rais Ruto watishia kutaja mali za Rais Uhuru

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Marafiki wa Naibu Rais William Ruto mnamo Alhamisi, Septemba 2, walitishia kufichua kile walichokitaja kama "biashara haramu za ardhi zinazohusishwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Swala la mali ya Ruto limzua mdahala kwa takriban siku mbili mfululizo baada ya Matiang'i kumuanika Bungeni wakati wa mvutano kuhusiana na ulinzi wake.

Wakiongozwa na Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua, wanasiasa hao walimsuta Waziri Fred Matiang'i kwa kutia chumvi utajiri alioanika akidai ni wa DPMwanasiasa huyo alitishia kuanika biashara haramu zinazodaiwa kuendeshwa na familia ya kiongozi wa taifa Uhuru.

Wakiongozwa na Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua, katika makaazi ya Ruto huko Karen Nairobi, wanasiasa hao walimsuta Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i kwa kutia chumvi utajiri alioanika akidai ni wa DP.

Gachagua, ambaye alionekana kukasirishwa na hatua ya Matiang'i alipofika mbele ya Bunge Jumatano, Septemba 1 alitishia kuanika biashara haramu zinazodaiwa kuendeshwa na familia ya kiongozi wa taifa.

"Matiang'i amefanya jambo nzuri kuanzisha mada kuhusu umiliki wa mashamaba...na sasa tutazamia swala hizo mzima mzima kwa sababu wametaka. Tunataka kujua ni nani alinyakua vipande vya ardhi ya Mau Mau huko Nakuru, ni nani anamiliki mashamba hayo na ni maafisa wangapi wa GSU wanayalinda?" Gachagua alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke