Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warundi watakiwa kutangaza utalii

3edb1bf6186a41fd9b73823e360696a0 Warundi watakiwa kutangaza utalii

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wa Burundi wametakiwa kusimama pamoja kutetea na kutangaza utalii wa nchi ili kuiwezesha sekta hiyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa kuingizia fedha nyingi za kigeni.

Wito huo ulitolewa na mwakilishi wa sekta ya utalii nchini, Leonidas Habonimana wakati wa mkutano na wajumbe wa sekta ya umma na binafsi kujadili maendeleo ya sekta hiyo na changamoto zinazoikumba mjini Bujumbura juzi.

“Wananchi wote wa Burundi bila kujali vyama, dini na makabila ni waathirika wa ukosefu wa watalii nchini. Hii inatokana na picha mbaya waliyonayo walimwengu kutoka kwa baadhi ya raia wasioitakia mema nchi na kuisema vibaya.”

“Burundi haipo katika vita, watalii waje tu kwa wingi kuitembelea na kujua vivutio vingi hapa nchini ambavyo havipatikani kokote duniani,” alisema Habonimana wakati akiwasilisha ujumbe wake kwa wadau wa utalii katika mkutano huo.

Alisema kuna nchi ambazo hazina amani kama ya Burundi lakini zinaendelea kupata watalii wengi.

“Watalii wanaothubutu kuja Burundi pamoja na mengi yanayosemwa wanarudi kwao wakiwa na picha nzuri kuhusu taifa letu na kuachana na uzushi wa watu wasioipenda nchi yao,” alisema.

Mwenyekiti wa taasisi binafsi inayojishughulisha na mambo ya utalii nchini, Faustin Ndikumana alisema haiingii akilini kusikia watu wakisema Burundi ni masikini wakati ina rasilimali za kutosha.

Chanzo: habarileo.co.tz