WANANCHI wa Burundi, leo wanatarajia kuapiga kura ya kuchagua rais, wabunge na madiwani.
Hatua hiyom inakaribia kumaliza utawala wa miaka 15 wa Rai Pierre Nkurunziza ambaye ameahidiwa kupewa nafasi ya kuwa “msahauri wa ngazi ya juu wa uzalendo “,
Pia atapokea malipo ya Dola za Marekani 540,000 na makazi ya kifahari. Lakini haijawa wazi ikiwa atatoweka katika hadharani na kutumia muda wake zaidi kwa mambo mengine mfano mchezo wa soka anaoupenda.
Mchakato wa kuelekea uchaguzi ambao wagombea saba wamejitokeza kuchua nafasi ya rais,umetawaliwa na gasia na shutuma kwamba uchaguzi hautakua wa haki na huru.
Lakini yoyote kwa atakayeshinda tatakiwa kisheria kupata ushauri kutoka kwa Rais Nkurunziza juu ya masuala ya usalama na umoja wa taifa. Kama watafuata ushauri wake bado halijawa wazi.
Ingawa anaweza kuwashawishi kwa kuonyesha mafanikio yake , kama vile kuanzisha elimu ya msingi bure, huduma bure za matibabu kwa wanawake na watoto, na kujenga barabara na hospitali.
Miaka mitano iliyopita, muhula watatu wa Rais Nkurunziza ulianza wakati taifa hilo likiwa katika kipindi cha ghasia za kisiasa. Tangazo lake angegombea kuwa rais kwa miaka mitano zaidi mamlakani lilichochea hasira ambapo baadhi walihoji uhalali wa hatua hiyo kisheria.
Kulikuwa na jaribio la mapinduzi, mamia ya watu walikufa katika makabiliano na maelfu wakalazimika kuikimbia nchi yao . Kuchaguliwa kwake Julai 2015, ambapo alipata karibu asilimia 70 ya kura, kulielezewa kama ‘’mzaha’’ na kiongozi wa upinzani nchini humo Agathon Rwasa, ambaye alisusia uchaguzi.
Burundi imerekodi visa zaidi ya 40 pekee vya maambukizi ya virusi vya corona, ikiwa na kifo kimoja, lakini busara ya kuendesha mikutano ya kisiasa ya umati wa watu imekua ikihojiwa.
Msemaji wa serikali alisema Machi, mwaka huu, wakati hakuna visa vilivyokua vimerekodiwa, kwamba nchi imelindwa na Mungu.
Burundi imekataa kuweka sheria kali, huku serikali ikiwashauri tu watu kuzingatia kanuni za usafi na kuepuka mikusanyiko pale inapowezekana-isipokua bila shaka mikutano ya kampeni za kisiasa.
Lakini serikali inasisitiza kuwa waangalizi wa kigeni wa uchaguzi watalazimishwa kutengwa kwa siku 14 kuanzia siku watakapowasili nchini, jambo linaloonekana kama njia ya kuwazuwia kwenda Burundi kabisa.
‘’Kile tulichokiona katika miezi michache iliyopita ni kwamba fursa ya kisiasa nchiniBurundi ni ndogo “ Nelleke van de Walle, anayefanyakazi katika taasisi ya utatuzi wa migogoro ya Afrika