Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani waliamsha, wataka Rais aondoke madarakani

Tunisia Uislamu Wapinzani waliamsha, wataka Rais aondoke madarakani

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wokovu wa Kitaifa Tunisia siku ya Jumanne kilimtaka Rais Kais Saied kuachia ngazi na kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mapema nchini humo.

Muungano mkuu wa upinzani ulisema katika taarifa kwamba Saied alishindwa "kupata idhini ya wananchi katika mradi wake wa mapinduzi" na hivyo kupoteza uhalali wa kusalia madarakani.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa asilimia 75 ya wapiga kura waliojiandikisha nchini Tunisia hawakupiga kura ya maoni iliyofanyika Jumatatu kuhusu katiba inayopendekezwa ya Saied.

Mkurugenzi wa taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Sigma Conseil alisema ni asilimia 25 pekee ya wapiga kura walishiriki katika kura ya maoni ya Julai 25 kuhusu katiba mpya.

Hassan Zargouni, akizungumza kwenye televisheni ya umma ya Tunisia, alisema asilimia 92.3 ya washiriki walipiga kura kuunga mkono rasimu ya katiba.

Bodi ya uchaguzi nchini humo, hata hivyo, ilisema waliojitokeza kupiga kura ni 27.5% ya wapiga kura wanaostahili.

Tunisia iko kwenye mzozo mkubwa wa kisiasa tangu Julai 25, 2021, wakati Saied alipoivunja serikali na kusimamisha bunge.

Vyama vya upinzani Tunisia vinachukulia hatua hizi kama "mapinduzi dhidi ya katiba," wakati wengine wanaziona kama "marekebisho ya mkondo wa mapinduzi ya 2011," ambayo yalimpindua Rais wa wakati huo Zine El Abidine Ben Ali.

Saied, ambaye alianza muhula wa urais wa miaka mitano mnamo 2019, anaamini kuwa hatua zake ni muhimu ili kuokoa nchi na kile alichokiita "hatari iliyokaribia."

Kupasishwa kwa katiba mpya nchini Tunisia kunamaanisha kuwa, Rais Kais Saied ataruhusiwa kuwasilisha miswada ya sheria na kuwa na mamlaka makubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live