Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani waandamana DRC, Risasi za moto zadaiwa kutumika

DR Congo 1 1 Wapinzani waandamana DRC, Risasi za moto zadaiwa kutumika

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wafuasi wa wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) wameandamana jana Jumatano Desemba 27, 2023 wakishinikiza uchaguzi uliofanyika Desemba 20, urudiwe.

Baadhi ya viongozi wa upinzani kwenye uchaguzi huo wamedai uligubikwa na udanganyifu mkubwa ukiwemo usogezwaji mbele wa siku za kupiga kura. Hivyo wanasema uchaguzi huo ni batili.

Tovuti ya DW imeripoti kuwa upinzani nchini humo unalalamikia kutumika kwa risasi za moto katika kutawanya maandamano hayo.

Polisi kwa upande wao wamesema hakuna risasi ya moto ilizotumika isipokuwa gesi za kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.

Chanzo: Mwanaspoti