Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani Zimbabwe wayakataa matokeo

Kinara Kinara Upinzani Zimbabwe Wapinzani Zimbabwe wayakataa matokeo

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa wa Zimbabwe ameshinda muhula wa pili na wa mwisho wa urais katika matokeo yaliyokataliwa na upinzani na kutiliwa shaka na waangalizi wa kieneo na kimataifa.

Mnangagwa ambaye ni maarufu kwa jina la "Mamba" aliingia madarakani kwa mara ya kwanza nchini Zimbabwe baada ya mapinduzi baridi yaliyomwondoa madarakani hayati Robert Mugabe mwaka 2017. Mwaka mmoja baadaye, alimshinda Chamisa kwa kura chache ambapo kiongozi huyo wa upinzani alilalalamika kuwa ni ulaghai mtupu.

Wachambuzi wa mambo walitabiri mapema ushindi wa wa Mnangagwa kwenye uchaguzi huo licha ya kuendelea msukosuko wa kiuchumi nchini humo. Wachambuzi hao walisema kuwa mazingira yaliyokuwepo tangu mwanzo yalikuwa ni kwa maslahi ya chama tawala cha ZANU-PF ambacho kinatawala Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipojikomboa na kupata uhuru wake tarehe 18 Aprili, 1980.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa usiku wa kuamkia leo na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), Mnangagwa ameshinda tena urais kwa kupata asilimia 52.6 ya kura ikilinganishwa na asilimia 44 ya Nelson Chamisa, mpinzani wake mkuu.

Wafuasi wa chama cha Zanu-PF cha Zimbabwe wakifurahia ushindi wa Mnangagwa

Sehemu moja ya taarifa ya Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Chigumba imesema: "Mnangagwa Emmerson Dambudzo wa chama cha ZANU-PF ametangazwa kuwa rais aliyechaguliwa kihalali wa Jamhuri ya Zimbabwe."

Waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Madola na SADC waorodhesha kasoro kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku mikutano ya wapinzani, masuala ya daftari la wapiga kura, matangazo ya vyombo vya habari vya serikali yenye upendeleo na vitisho kwa wapiga kura.

Kwa upande wake, Promise Mkwananzi, msemaji wa Chama cha Wananchi cha Chamisa (CCC) amesema kuwa chama hicho hakikutia saini matokeo ya mwisho, ambayo ameyataja kuwa ni ya "uongo."

Uchaguzi huo ulikumbwa na ucheleweshaji uliochochea shutuma za upinzani za wizi na ukandamizaji wa wapiga kura lakini kundi dogo la wafuasi wa chama tawala walisherehekea matokeo siku ya Jumamosi.

Lakini Promise Mkwananzi, msemaji wa Chama cha Wananchi cha Chamisa (CCC) alisema chama hicho hakijatia saini matokeo ya mwisho, ambayo aliyataja kuwa ya "uongo".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live