Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani Senegal wataka Ousmane Sonko aachiwe huru

Sonko Kitabuni Kura Wapinzani Senegal wakaribisha kuachiwa huru kwa Ousmane Sonko

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafuasi wa kambi ya upinzani nchini Senegal wamekaribisha hatua ya kuachiwa huru kiongozi wa kambi hiyo, Ousmane Sonko, aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kumkashifu Waziri wa Utalii, Mame Mbaye Niang.

Maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani walimiminika kwenye mitaa ya Dakar, wakiimba jina la Sonko barabarani nje ya nyumba yake. Wengine waliwasha moto, kucheza au kupiga honi za pikipiki na magari yao.

"Tumekuwa tukingojea siku hii kwa muda mrefu”, amesema mfanyakazi wa afya mwenye umri wa miaka 52, ambaye ametaja jina lake la kwanza la Fatima pekee. "Ninaamini Sonko anaweza kubadilisha nchi', amesema mwandamanji huyo.

Shirika la utangazaji la Senegal, RTS, limeripoti kuwa Sonko ameachiliwa huru pamoja na mshirika wake mkuu, Bassirou Diomaye Faye.

Kuachiliwa huru kwao kunakuja baada ya mzozo uliosababishwa na uamuzi wa Rais Macky Sall kuahirisha uchaguzi wa urais wa Februari 25 na ni jambo lililotarajiwa baada ya kupitishwa sheria ya msamaha wiki iliyopita kwa vitendo vilivyohusiana na maandamano ya kisiasa tangu 2021.

Uchaguzi huo, ambao serikali ilitaka uahirishwe kwa miezi 10, sasa unatarajiwa kufanyika Machi 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live