Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani Comoro wasema chama tawala kimependelewa katika uchaguzi

Wapinzani Comoro Wapinzani Comoro wasema chama tawala kimependelewa katika uchaguzi

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagombea watano wa upinzani katika uchaguzi wa rais wa Jumapili wa Comoro wamesema zoezi la upigaji kura limekumbwa na "udanganyifu" na "kujaza masanduku ya kura" huku Rais Azali Assoumani akiwa imani kwamba atashinda moja kwa moja katika duru ya kwanza na hivyo kuendelea kutawala visiwa hivyo..

Mouigni Baraka Said Soilihi akiwa ameandamana na wagombea wengine wa urais amesema katika taarifa kwamba: "Kama mwaka wa 2019, tunashuhudia udanganyifu katika udaganyifu unaofanywa na Azali Assoumani na ushirikiano wa jeshi."

Viongozi hao wa upinzani wanadai kuwa tume ya uchaguzi inapendelea chama tawala, suala ambalo tume imekanusha na kusema kwamba zoezi la upigaji kura limekuwa na uwazi.

Uchaguzi wa Comoro umefanyika Jumapili ambapo Rais Assoumani anatarakiwa kupata ushindi kwa wa muhula wa nne wa miaka 5. Rais Assoumani

Zoezi la upigaji kura lilianza kwenye visiwa hivyo vya bahari Hindi saa 2 za asubuhi, likishirikisha wapiga kura 338,940 waliojiandikisha kati ya jumla ya wakazi 800,000 nchini humo.

Upigaji kura ulimalizika saa 12 za jioni kwenye taifa hilo ambalo limeshuhudia takriban majaribio 20 ya mapinduzi, tangu kupata uhuru wake kutoka ka Ufaransa mwaka 1975.

Rais Assoumani amesema anatumai kushinda katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi.

"Kuna imani kwamba nitashinda kwenye duru hii ya kwanza. Ni Mwenyezi Mungu ndiye atakayeamua na watu wa Comoro," alisema rais Assoumani baada ya kupiga kura kwenye kitongoji kimoja nje kidogo ya mji mkuu Moroni.

Rais Assoumani -- ambaye amekuwa akiwakandamiza wapinzani wake kwa mkono wa chuma ikiwemo kuwafunga jela na kuwalazimisha wengine kwenda uhamishoni-- amekanusha madai ya dosari kwenye uchaguzi huo.

Miongoni mwa dosari zilizotajwa ni hitilafu kwenye vituo vya kupigia kura ambazo amesema "hajazisikia" na kuhusu idadi ndogo ya wapigakura waliojitokeza, rais Assoumani alisema hilo limechangiwa na hali mbaya ya hewa husasani mvua iliyokuwa inanyesha jana Jumapili.

Zoezi la kuhesabu kura lilianza punde baada ya vituo kufungwa. Matokeo ya uchaguzi huo wa jana yanatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha siku chache zijazo.

Rais Assoumani ambaye anatawala visiwa vya Comoro tangu mwaka 2016 alirefusha muhula wake madarakani kupitia mabadiliko tata ya katiba.

Mabadiliko ya katiba ya baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2019 yaliyoondoa sharti la nafasi ya urais kuwa ya kupokezana miongoni mwa visiwa vitatu vikubwa vinavyounda Jamhuri ya Comoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live