Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiganaji wa Taureg wateka kambi ya nne ya jeshi la Mali

Wapiganaji Wa Taureg Wateka Kambi Ya Nne Ya Jeshi La Mali Wapiganaji wa Taureg wateka kambi ya nne ya jeshi la Mali

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Voa

Wapiganaji wa kabila la Taureg kaskazini mwa Mali walitangaza Jumapili kwamba, wameteka kambi nyingine ya kijeshi kutoka jeshi la Mali kufuatia mapigano kaskazini mwa nchi hiyo.

Hiyo imekua kambi ya nne kutekwa kutokana na mfululizo wa mashambulizi yanaofanywa na mungano wa waasi unaofahamika kama Coordination of Azawaad Movements (CMA), tangu mwezi Ogusti baada ya kuondoka kwa kikosi cha Amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, ambacho kiliweza kusaidia kudumisha kwa sehemu fulani utulivu kwa miaka kadhaa katika nchi hiyo.

Mohamed Elmaouloud Ramadane msemaji wa CMA ameliambia shirika la habari la Reuters Jumapili, kwamba wamechukua udhibiti wa kambi ya jeshi ya Bamba katika jimbo la Gao, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Jeshi la Mali upande wake limesema kwenye ukurasa wake wa X, kwamba mapigano makali yamekua yaliendelea huko Bamba na kwamba maelezo zaidi yatatolewa baadae.

Shambulio la CMA huko Bamba linalofuatia mashambulio kwenye kambi za Lere, Dioura, na Bourem katika wiki chache zilizopita, ni ishara ya kuongezeka mapigano wakati pande zote mbili zikijaribu kuchukua udhibiti wa maeneo ya janga la kati na kaskazini ya taifa hilo la Sahel, mara tu baada ya kuondoka kwa Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Mali limekuwa pia likishambuliwa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya al Qaeda na Islamic State.

Wataureg kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kwamba serikali haijashughulikia maslahi yao na wamekua wakipigania uhuru wa jimbo lao la jangwani wanaloliitia Taifa la Azawad.

Chanzo: Voa