Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiganaji wa LSM wajiunga na jeshi la Sudan dhidi ya RSF

Jeshi La Sudan Linasonga Mbele Na Kuuteka Mji Wa Omdurman Wapiganaji wa LSM wajiunga na jeshi la Sudan dhidi ya RSF

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Minni Arko Minawi, mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan (SLM) ambaye pia ni gavana wa jimbo la Darfur, ametangaza kuwa vikosi vya harakati hiyo vinaelekea katika mji mkuu, Khartoum, kushirikiana na jeshi la taifa katika mapambano dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Minawi amerusha kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa pamoja na vikosi vyake na kusema: "Tuko njiani kuelekea mji mkuu, Khartoum."

Kiongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan (SLM) amesema: "Tunaishi katika mzozo ambao unatokana na shambulio dhidi ya Serikali, haki na utu wa raia, na mamlaka ya Serikali katika maeneo mengi ya nchi."

Ameendelea kusema kuwa, "SLM ilisubiri miezi 10 tangu kuanza kwa vita ili kupatikane suluhisho, lakini hilo halikufanyika, hivyo harakati hii lazima ichangie katika kurejesha mali za watu na kurejesha mamlaka ya nchi kutoka kwa wale wanaotoka katika nchi mbalimbali (RSF)."

Tangu katikati ya Aprili 2023, jeshi la Sudan likiongozwa na mkuu wa Baraza la Mpito la Utawala, Abdel Fattah al-Burhan, limekuwa katika vita vikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo, na hadi sasa mapigano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 13,000 na takriban milioni 8.5 wamelazimika kuwa wakimbizi ndani ya nje ya Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live