Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiganaji 50 wa Boko Haram wauawa na Jeshi la Niger

Boko Haramu Wapiganaji 50 wa Boko Haram wauawa na Jeshi la Niger

Fri, 27 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapiganaji hamsini wa kikundi cha Boko Haram wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapambano kati yao na jeshi la Niger katika kijiji cha Baroua kinachohifadhi wakimbizi wa ndani.

Waziri wa Ulinzi ya nchi hiyo, Alkassoum Indatou, amewaambia waandishi wa habari kuwa askari kumi na sita wa jeshi la serikali wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa katika mapambano hayo.

Zaidi ya watu 30,000 wameuawa na milioni 2 wameyakimbia makazi yao tangu kulipoanza uasi wa kundi hilo mwaka 2009, hii ikiwa ni kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, pamoja na jopo la wataalamu lililojikita New York, linaloangazia masuala ya mahusiano ya kimataifa, CFR.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live