Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiganaji 14 wa uasi warejeshwa Uganda

Uasi Warejeshwa.jpeg Wapiganaji 14 wa uasi warejeshwa Uganda

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uganda imepokea wapiganaji 14 wa zamani wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army (LRA) wanaopigania kusimamia amri 10 za Biblia waliorejeshwa makwao kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Kundi la kwanza la waasi hao wa zamani wakiongozwa na Meja Jenerali Ali Acaye, maarufu kwa jina la "Doctor," pamoja na wake zao 14 na watoto 33 ambao walikuwa wamejificha kwenye misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, waliwasili siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, ulioko umbali wa kilomita 40 kusini mwa Kampala, mji mkuu wa Uganda, kwa ndege ya kukodi.

Wanachama wa kundi hilo la Kikristo la waasi wa LRA waliojisalimisha kwa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mjini Bangui wamepokewa na Waziri Mkuu wa Uganda, Robinah Nabbanja katika kambi ya kijeshi ya Entebbe.

Waziri Mkuu wa Uganda, Robinah Nabbanja (katikati) akisalimiana na Meja Jenerali Ali Acaye Nabbanja amesema: “Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyefanikisha zoezi hili la kuwapokonya silaha, kuwaondoa msituni na kuwarejesha makwao wananchi wenzetu wa Uganda. Karibuni nyumbani. Ofisi yangu itafanya kazi na washikadau wengine kukusaidieni kujumuika na kuishi kwa salama katika jamii zenu."

Zoezi la kuwarejesha makwao waasi hao wa zamani wa LRA limefanikishwa na mashirika ya ndani na ya nje ya Uganda. LRA ni kundi la Kikristo linalopigania kuipindua serikali iliyopo madarakani na kusimamisha serikali ya Kikristo inayoendeshwa na Amri Kumi za Biblia. Genge hilo ni maarufu sana kwa kufanya jinai za kila namna katika uasi uliodumu kwa miaka 20 sasa. Wameua makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia, kuwataka viungo baadhi yao, kuwateka nyara zaidi ya watoto 20,000 na kuwaingiza vitani kwa nguvu, kuendesha utumwa wa ngono, na kupelekea zaidi ya watu milioni 1.8 wa kaskazini mwa Uganda, kuwa wakimbizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live