Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiga Kura wa Liberia Kumchagua rais wake Jumanne

Wapiga Kura Wa Liberia Kumchagua Rais Wake Jumanne Wapiga Kura wa Liberia Kumchagua rais wake Jumanne

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Voa

Waliberia watapiga kura siku ya Jumanne katika uchaguzi wa marudio kati ya Rais George Weah na makamu wa rais wa zamani Joseph Boakai baada ya kupambana vikali katika duru ya kwanza ambapo hakuna mgombea aliyeweza kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazotakiwa ili kupata ushindi wa moja kwa moja.

Nyota wa zamani wa soka Weah aliongoza duru ya kwanza, kwa kupata asilimia 43.83 ya kura, na Boakai alipata asilimia 43.44.

Tofauti ndogo ya kura kati yao, na kutokuwepo kwa mgombea wa tatu mwenye nguvu, inamaanisha kuwa duru ya pili pia itakuwa na ushindani mkubwa, alisema Maja Bovcon, mchambuzi mkuu wa Afrika katika kampuni ya ujasusi ya Verisk Maplecroft.

Duru ya pili ni kama marudio ya mwaka 2017 ambapo Weah, alipata fursa ya wimbi la umaarufu, alimshinda Boakai kwa asilimia 61.54.

Alishinda kwa ahadi ya kukabiliana na ufisadi na kuboresha maisha katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo bado linaibuka kutoka katika vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989 na mwaka 2003, na janga la Ebola la 2013 hadi 16 ambalo liliua maelfu ya watu.

Lakini baadhi ya wapiga kura wamechukizwa na kitendo cha Weah kushindwa kutekeleza ahadi zake, hususani rushwa, kiwango cha juu cha vijana wasi na ajira, mfumuko wa bei ya vyakula, na matatizo ya kiuchumi kwa ujumla.

Weah amelilaumu janga la virusi vya corona na matokeo ya vita vya Russia na Ukraine kwa kushindwa kuuweka uchumi katika malengo. Chanzo cha habari hi ni Shirika la habari la Reuters.

Chanzo: Voa