Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapenzi wanaswa wakila uroda kanisani Uganda

Wapenzi Wanaswa Wakila Uroda Kanisani Uganda Wapenzi wanaswa wakila uroda kanisani Uganda

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wakaazi wa wilaya ya Bugonya nchini Uganda wameapa kutosali katika Kanisa moja katika eneo hilo baada ya wanandoa kupatikina wakishiriki tendo la ndoa kwenye madhabahu ya kanisa hilo.

Viongozi wa kanisa hilo katika Kata Ndogo ya Kayonza Wilaya ya Kayonza sasa wanasema wameingia katika idadi isiyojulikana ya siku za kufunga na sala kufuatia kile walichokielezea kuwa ni kitendo cha kushtua.

Siku ya Jumatano, wenyeji waliiambia tovuti ya Monitor kwamba wataepuka kanisa hilo hadi viongozi wake waandae misa maalum ya kusafisha "kitendo cha kishetani kilichotokea nyumbani kwa Mungu Jumanne mwendo wa saa 8 jioni."

Mwenyekiti wa Bugonya IC1 George William Kanda alieleza kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji chake aliingia kanisani na mwanamke Muislamu kupitia dirisha.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wapenzi hao waliweza kuingia katika kanisa hilo kupitia madirisha kwa sababu milango ilikuwa imefungwa.

"Walifika kanisani kupitia madirisha sababu milango wa kanisa ilikuwa imefungwa," Kanda alisema.

Cha kushangaza Zaidi ni kuwaWawili hawa hawakuwa washirika wa kanisa hilo bali wanakijiji katika eneo hilo.

Chanzo: Radio Jambo