Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapenzi wadaiwa kumuuza mtoto wao ili wanunue dawa

Joy Umukoro 636x365 Wapenzi wadaiwa kumuuza mtoto wao ili wanunue dawa

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu cha Jimbo la Edo nchini Nigeria, kimewatia mbaroni mwanaume mwenye umri wa miaka 48, Anthony Igbinogun na mpenzi wake, Joy Umukoro, 28, kwa madai ya kumuuza mtoto wao wa mwezi mmoja ili kununua dawa ambazo haijawekwa wazi ni dawa za aina gani.

Washukiwa hao walikamatwa wakiwa na rafiki yao, Precious James mwenye umri wa miaka 26, ambaye aliripotiwa kuwezesha shughuli hiyo haramu na kuwaunganisha wanandoa hao na mnunuzi huko Port Harcourt, Jimbo la Rivers.

Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi maalumu wa kukabiliana na biashara hiyo haramu ya uuzaji binaadamu, Abigail Ihonre, ambaye alizungumza haya Ijumaa, Juni 23, 2023, nchini Benin, alisema kuwa mtoto huyo aliuzwa kwa Naira milioni 1.7 ambayo kwa pesa za Tanzania ni sawa na shilingi milioni 4.9.

"Uchunguzi wetu ulibaini kuwa Joy Umukoro, mama wa mtoto huyo, alijifungua mtoto mnamo Aprili 2023, na kula njama na mpenzi wake kumuuza mtoto wao kwa Naira milioni 1.7 . Amekiri kosa la kumuuza mtoto mchanga.”

Alisema uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea ili kuwapata wanunuzi na mtoto, na kuongeza kuwa kila mtu ambaye ana hatia atachukuliwa hatua za kisheria.

Bado tunazidi kufuatilia mkasa huu na pindi tutakapo pata taarifa zaidi tutakujuza kipi kinaendelea usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live