Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapenda kulala? Kampuni yatangaza nafasi za kazi ya kulala na kulipwa KSh150K

0fgjhs3fvbc3sqak8g Wapenda kulala? Kampuni yatangaza nafasi za kazi ya kulala na kulipwa KSh150K

Wed, 12 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Eachnight inawatafuta watu wa kujiunga na kikosi cha utafiti kama weledi wa kulala

- Weledi hao wa kulala watatumika katika utafiti wa kubaini umuhimu wa usingizi na hasara yake

- Kila mweledi wa usingizi atalipwa KSh 159,000 baada ya siku 30 ya utafiti huo

Kampuni moja nchini Marekani ambayo hutoa vidokezo vya usingizi imetangaza nafasi za kazi ya weledi wa usingizi.

Kampuni ya Eachnight ilisema inawatafuta watu wa kujiunga na kikosi cha utafiti kama weledi wa kulala kubaini umuhimu wa usingizi na hasara yake.

"Kwa sasa tunaajiri kikosi cha watu watano ambao watakuwa weledi wa usingizi na kulipwa kulala! Pia hatufanyi matani," ilisema kampuni hiyo kwenye tovuti yake.

Kampuni hiyo iliwaomba wale ambao wangelipenda kuwa sehemu ya utafiti huo kuwasilisha maombi yao mtandaoni kabla ya Mei 31, 2021.

Watakaofaulu kupata kazi hiyo watalipwa KSh 159,000 na wataanza punde baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha siku 30 za utafiti huo.

Watakaotuma maombi ni lazima walale pekee yao wakati wa kipindi hicho ili kuhakikisha kuwa usingizi wao haukatizwi.

Wakati wa utafiti huo, watafiti watabaini muda mwafaka wa kulala na athari za kulala sana hadi kuchoka.

Mambo mengi watakayozingatia ni athari za usingizi kwa kumbukumbu, motisha na tija

Kama sehemu ya utafiti na kufaulu kwake, kutakuwa na simu za video baada na wakati wa utafiti na kuulizwa maswali ya moja kwa moja ambapo weledi wa usingizi wataelezea ushuhuda wao.

Katika taarifa sawia na hiyo ya TUKO.co.ke, mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 21, ambaye aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kulala na alishindwa kulala kwa wiki tatu.

Rhoda Rodriguez, ana ugonjwa wa kulala ambao unajulikana kama Kleine-Levin Syndrome.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke