Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waombolezaji wamiminika kwenye mazishi ya kiongozi mtata wa Wazulu

Waombolezaji Wamiminika Kwenye Mazishi Ya Kiongozi Mtata Wa Wazulu Waombolezaji wamiminika kwenye mazishi ya kiongozi mtata wa Wazulu

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Waombolezaji wamefika katika mji wa Ulundi kabla ya mazishi ya Jumamosi ya mwanasiasa mkongwe wa Afrika Kusini na chifu wa Wazulu Mangosuthu Buthelezi.

Amepewa mazishi ya kitaifa kwa heshima kwa mchango wake katika vita dhidi ya utawala wa wazungu wachache.

Kama ishara ya heshima, kampuni ya kitaifa ya umeme pia imekubali, eneo la Ulundi halitakabiliwa na mgao wa umeme kitaifa wakati wa mazishi yake.

Lakini kifo chake akiwa na umri wa miaka 95 kimefungua mjadala kuhusu urithi wake.

Alizaliwa katika familia ya kifalme ya Wazulu, na aliendelea kuwa waziri mkuu wao wa jadi hadi kifo chake. Hata hivyo, ni jukumu lake katika siasa ambalo limesababisha mgawanyiko.

Alianzisha chama cha Zulu cha Inkatha Freedom Party (IFP) baada ya kukatishwa tamaa na chama cha African National Congress (ANC) mwaka wa 1975 katika kilele cha utawala wa kibaguzi. Alipinga msimamo wa ANC kuhusu hatua za kutumia silaha na vikwazo, akisema kuwa viliwadhuru Waafrika Kusini weusi.

Kwa hili, wafuasi wake wanaamini kuwa anastahili sifa zote anazomiminiwa - na mamia ya watu waliojipanga barabarani siku ya Ijumaa kuelekea Ikulu ya Kwa-Phindangene huko Ulundi, pamoja na waimbaji wa nyimbo za sifa za Kizulu wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni wanamuona kama mtu wa amani.

Prof Kealeboga Maphunye, mkuu wa siasa za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini, anakiri kwamba Buthelezi alikuwa "kiongozi wa kimila anayeheshimika ambaye alitoa mchango mkubwa katika historia kwenye kuhakikisha kwamba utu wa watu weusi, hasa Wazulu, haukandamizwi na utawala wa kibaguzi" .

Chanzo: Bbc