Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waombeeni viongozi wenu watimize mapenzi ya Mungu, DP Ruto awarai Wakenya

Ce7ee4af35ff3c2b Waombeeni viongozi wenu watimize mapenzi ya Mungu, DP Ruto awarai Wakenya

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Naibu Rais William Ruto alituma ujumbe maalum kwa Waislamu wakati wa mfungo wa Ramadhan

- DP alisema kipindi hiki ni fursa kwa Waislamu kuungana na wenzao kutoka madhehebu mengine kuiombea nchi

- Pia aliwaomba Wakenya kuzingatia itifaki za COVID-19 zilizowekwa na serikali

Naibu Rais William Ruto ametoa wito kwa Wakenya kuwaombea viongozi wao wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa kivumbi cha siasa mwaka ujao.

Katika ujumbe wake maalum kwa Waislamu wakati huu wa mfungo wa Ramadhan, Ruto aliwahimiza Wakenya kutoka madhehebu mengine kujiunga na jamii ya Waiskamu kuliombea taifa.

Alitaka Wakenya wote kutoka kona zote za nchi kuwa na amani na umoja miongoni mwao.

"Wacha tuendelee kudumisha amani na umoja kwa sababu taifa hili ni letu sote. Tuwaombee viongozi wote bila kujali mrengo wao wa siasa. Tuombeeni ili tuweze kutimiza mapenzi ya Mungu katika nchi yetu," alisema.

DP alitambua umuhimu wa kipindi cha mfungo cha Waislamu, akiongeza kuwa ni nguzo thabiti katika dini.

"Imeelezwa katika Qur'ani kwamba Mwenyezi Mungu anasema" Enyi mlioamini, fungeni mlivyoamriwa kama wale waliokuwepo kabla yenu walivyiofanya, ili mpate kumjua Mungu, " alisema Ruto.

Ruto pia alichukua nafasi hiyo kuwasihi Wakenya kuzingatia itifaki zilizoidhinishwa na Rais Uhuru Kenyatta katika harakati za kupambana na kuenea kwa COVID-19.

Alisema maagizo hayo yalilenga kukabiliana na virusi vya kutisha na pia aliwahimiza Wakenya kutemeblea vituo vya afya vilivyoko karibu nao kupokea chanjo ya AstraZeneca COVID-19.

Waislamu walianza kipindi cha siku 30 cha kufunga wakati wa Ramadhan Jumatatu, Aprili 12.

Katika kipindi hicho, watakuwa wakifunga kuanzia majira ya jioni hadi alfajiri, lengo lao ni kumkaribia Mungu kwa njia ya sala na tafakari.

Mfungo wa mwaka huu unatarajia kukamilika Mei 11 baada ya mwezi kuonekana.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke