Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyamapori wanaogopa sauti za binadamu kuliko mngurumo wa simba - utafiti

Wanyamapori Wanaogopa Sauti Za Binadamu Kuliko Mngurumo Wa Simba   Utafiti Wanyamapori wanaogopa sauti za binadamu kuliko mngurumo wa simba - utafiti

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Utafiti nchini Afrika Kusini umegundua kuwa sauti za binadamu husababisha hofu zaidi kwa mamalia wa mwitu kuliko sauti ya simba.

Wanasayansi walicheza rekodi za watu wakizungumza kawaida kupitia spika zilizofichwa kwenye mashimo ya maji katika mbuga ya kitaifa ya Kruger.

Takriban 95% ya wanyama wakiwemo swara, nguruwe, twiga na chui waliogopa sana na kukimbia haraka.

Rekodi za simba wanaonguruma zilisababisha wasiwasi mdogo sana; tembo wengine walijibu kwa kujaribu kutishia chanzo chasauti za paka mwitu.

Inadhaniwa wanyama hao wamejifunza kuwa kuwasiliana na binadamu ni hatari sana, kutokana na kuwinda, kutumia bunduki na kutumia mbwa kuwakamata.

Chanzo: Bbc