Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyama apishana na Samatta Uingereza, atua Ligi Kuu Marekani

97864 Pic+wanyama Wanyama apishana na Samatta Uingereza, atua Ligi Kuu Marekani

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Kiungo wa Tottenham, Victor Wanyama amejiunga na klabu ya Montreal Impact baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha klabu hiyo ya London kaskazini.

Kiungo huyo raia wa Kenya mwenye umri miaka 28 amejiunga na Impact kwa uhamisho huru akisaini mkataba wa miaka mitatu.

Wanyama atajumuika na wenzake Impact mara atakapokamilisha vipimo vya afya na uhamisho wake wa kimataifa kukamilika.

Amezungumzia furaha yake ya kuanza maisha mapya pamoja na kocha maarufu wa Impact, nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, ambako atakuwa mchezaji wa pili supastaa pamoja na kiungo mwenzake, Saphir Taider.

"Nina furaha kujiunga na nzuri kama hii ya Montreal Impact," Wanyama alisema.

"MLS (Ligi Kuu ya Marekani) inaendelea kukua kila siku na natarajia kuitangaza klabu hii, mjini hapa na kote Afrika.

"Nilipozungumza na Thierry na aliponiambia kwamba anahitaji nijiunge naye Montreal, sikufikiria mara mbili. Yeye alikuwa ni mchezaji ambaye daima nilikuwa nikivutiwa naye, na nina furaha kupata fursa ya kufanya kazi naye na kutoa mchango utakaowezesha Montreal Impact iongezeke ubora na natumai tufikie hatua ya juu ya michuano tunayoshiriki.

"Nadhani familia ya Saputo na menejimenti ya timu ya Montreal wana plani nzuri na natumai nitatoa mchango mkubwa wa kufanikisha mpango huu."

Wanyama alijiunga na Tottenham mwaka 2016 - baada ya misimu mitatu ya kukiwasha Southampton - na akawa nguzo muhimu katika dimba la kati la kikosi cha kocha Mauricio Pochettino.

Alicheza mechi 97 za Spurs katika misimu minne, huku sehemu kubwa ya mechi hizo akicheza katika msimu wake wa kwanza kabla ya majeraha ya goti kumweka nje ya uwanja mfululizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz