Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wauawa katika shambulio la Al Shabab nchini Kenya

Viongozi Wa Kenya, Ethiopia Na Djibouti Kujadili Mashambuli Dhidi Ya Al Shaabab Wanne wauawa katika shambulio la Al Shabab nchini Kenya

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne, wakiwemo maafisa watatu wa polisi, waliuawa Jumatatu katika shambulizi lililohusishwa na wanamgambo wa itikadi kali wa Al Shabab katika mji wa mashariki mwa Kenya unaopakana na Somalia, polisi imesema siku ya Jumanne.

Mlipuko wa kilipuzi ulitokea katika hoteli iliyo umbali wa mita 200 kutoka kituo cha polisi huko Mandera mwendo wa 4:20 asubuhi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti. Kulingana na polisi, watu wanne, wakiwemo maafisa watatu wa polisi, waliuawa na karibu kumi wengine kujeruhiwa.

"Tunashuku kuhusika kwa Al shabab katika tukio hili," chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne. "Operesheni kubwa ya usalama inaendelea pamoja na uchunguzi wa kuhusika kwa watu ambao Al Shabab inafanya kazi nao ndani ya nchi," chanzo hiki kimeongeza. Kulingana na vyombo vya habari nchini, askari wawili wa akiba pia waliuawa wikendi iliyopita katika uvamizi katika kaunti ya Lamu, eneo lingine la mpaka wa Somalia.

Kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda, Al Shabab limekuwa likiongoza uasi mbaya kwa zaidi ya miaka 16 unaolenga kupindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na kuanzisha sheria za Kiislamu. Tangu uingiliaji wake wa kijeshi kusini mwa Somalia mwaka wa 2011 na kisha ushiriki wake katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom, sasa Atmis) iliyoundwa mwaka 2012 kupambana na uasi huu, nchi jirani ya Kenya pia imekuwa ikilengwa na kundi hili, ambalo pia linaajiri vijana kutoka nchini Kenya.

Mashambulizi mabaya yalilenga kituo cha biashara cha Westgate katika mji mkuu Nairobi mnamo mwezi wa Septemba 2013 (waliofariki 67), Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015 (waliofariki 148) na hoteli ya Dusit, pia jijini Nairobi, Januari 2019 (waliofariki 21). Mashambulizi ya kiwango cha chini bado yanafanyika mara kwa mara katika kaunti za Lamu, Mandera na Garissa, zilizo kwenye mpaka wa kilomita 700 kati ya nchi hizo mbili.

Serikali ya Somalia imekuwa ikiongoza mashambulizi dhidi ya Al Shabab katikati mwa Somalia tangu mwezi wa Agosti 2022, ikiwa na wanamgambo wa kikoo na usaidizi wa anga kutoka kwa jeshi la Marekani na Atmis. Baada ya kudhibiti tena baadhi ya maeneo, imekwama katika miezi ya hivi karibuni. Al Shabab sasa wanafanya mashambulizi ya kuvizia ndani ya nchi na nchi jirani ya Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live