Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wapoteza maisha wakielekea mkutano wa Raila

A95de6df6ca62c5b Wanne wapoteza maisha wakielekea mkutano wa Raila

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wingu la simanzi limetanda eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa baada ya wafanyakazi wanne katika afisi ya mbunge kurafiriki dunia.

Wanne hao walikuwa wakielekea Lamu kuhudhuria kikao cha kinara wa ODM Raila Odinga. Gari lao lilipata panchari na kupoteza mwelekeo kabla ya kubingiria mara kadhaa na kuwajeruhi vibaya wanne haoKifo chao kimetajwa kama pigo kubwa kwa Mbunge Nassir na uongozi wa Mvita

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir alisema wanne hao wlaifariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata punchari.

Walipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa na kusababisha vifo vya dereva papo hapo na kisha watatu wakakata roho wakikimbizwa kupata matibabu.

Ajali hiyo ilifanyika mkatika eneo la Mpeketoni, Lamu, wakati wa wanne hao kuelekea eneo ambalo kinara wa ODM Raila Odinga ana kikao.

Chama cha ODM kilituma rambirambi zake kwa familia za wanne hao baada ya ajali hiyo.

"Tumehuzunishwa na kifo cha wafanyakazi wanne wa Mbunge Nassir Ali Omar Naaman, Carol Wayua Mueni, Athman Mohammed Omar na Elysian Musyoka kupitia ajali ya barabara. Tunaombea familia ya waliofariki dunia kipindi hiki kigumu," ODM ilisema.

Gavana Hassan Joho alikuwa mmoja wa viongozi ambao walituma rambirambi zao kwa Abdulswamad.

Mwanaiaji wa ugavana Suleiman Shahbal alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa uongozi wa Mvita.

"Nimeshtushwa na kusikitishwa na habari za vifo vya wafanyakazi wa karibu wa ndugu yangu Abdulswamad Nassir akiwemo Mzee wetu Ali Naaman, Carol Wayua, Elyson Musyoka na Athman Mobammed.

Natoa rambi rambi zangu kwa familia za wote waliotuacha jioni ya leo na nawaombea Mungu awape subra wakati huu mgumu," alisema.

Alimtaja mzee Naaman kama aliyewavunja mbavu wengi na hivyo kuishia kuwa kipenzi cha wengi.

Naaman alikuwa mzee mcheshi na mtu wa watu aliyekuwa anependwa na kuheshimika na wengi wakiwemo wadogo na wakubwa.

Kazi yake, ukarimu na busara yake ilipelekea kupendwa kwake na wengi," alisema Shahbal

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke