Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wahukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanasiasa wa Tunisia Chokri Belaid

Wanne Wahukumiwa Kifo Kwa Mauaji Ya Mwanasiasa Wa Tunisia Chokri Belaid Wanne wahukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanasiasa wa Tunisia Chokri Belaid

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Tunisia imewahukumu watu wanne kifo na wengine wawili kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kiongozi mashuhuri wa kisiasa Chokri Belaid mwaka 2013.

Alipatikana ameuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake katika mji mkuu, Tunis, na kusababisha vurugu.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kushoto alikuwa mkosoaji mkali wa chama tawala cha Kiislamu cha Ennahda.

Alidai kuwa ilifumbia macho unyanyasaji unaofanywa na watu wenye itikadi kali dhidi ya watu wasiopenda dini.

Ingawa Tunisia inatoa hukumu za kifo kwa uhalifu mbaya zaidi, hakuna hukumu ya kifo iliyotekelezwa tangu 1990.

Badala yake, kwa kawaida hubadilishwa hadi kifungo cha maisha.

Jumla ya watu 23 wamefunguliwa mashtaka kuhusiana na mauaji ya Belaid.

"Haki imetendeka," Mwendesha Mashtaka Aymen Chtiba alisema akijibu hukumu hizo sita zilizotolewa Jumatano asubuhi.

Uamuzi huo ulitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa baada ya masaa 15 ya kujadiliwa, linaripoti shirika la habari la AFP.

Wanajihadi wenye utiifu kwa Islamic State walidai kuhusika na mauaji ya Belaid, pamoja na yale ya Mohamed Brahmi, kiongozi mwingine wa upinzani wa mrengo wa kushoto, miezi sita baadaye.

Mauaji haya yalisababisha maandamano makubwa kutoka kwa Watunisia waliokasirishwa, miaka miwili baada ya vuguvugu la demokrasia la Arab Spring kuanza nchini humo na kuenea mahali pengine katika Mashariki ya Kati.

Tunisia sasa inatawaliwa na Rais Kaïs Saïed, ambaye mwenyewe ametajwa kuwa ni mbabe baada ya msururu wa unyakuzi wa madaraka ikiwa ni pamoja na kuvunja chombo kikuu cha sheria nchini humo, kumfukuza waziri mkuu na kulivunja bunge.

Chanzo: Bbc