Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne familia moja wafariki kwa ajali ya Pikipiki

Wawili Wafariki Ajali Ya Pikipiki Kugonga Gari Wanne familia moja wafariki kwa ajali ya Pikipiki

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wa familia moja wamefariki papo hapo katika ajali mbaya ya barabarani, iliyohusisha usafiri wa umma maarufu kama Matatu na Pikipiki eneo la Vipingo kaunti ya Kilifi Nchini Kenya.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo, wamesema gari hilo la matatu lilikuwa likitoka njia ya Mombasa kuelekea barabara ya Kilifi na liligongana ana kwa ana na Pikipiki hiyo. Barabara App kusaidia ujenzi miundombinu, kupunguza ajali

Wamesema Pikipiki iliyohusika katika ajali hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Baba aliyekuwa amewabeba mkewe na watoto wawili, ambao wote waliaga dunia hapo hapo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika eneo hilo limesema linafuatilia chanzo cha ajali hiyo na watatoa taarifa kamili na majina ya waliofariki katika ajali hiyo mbaya iliyoangamiza familia, huku likiwasihi madereva wa vyombo kuwa makini barabarani wakati wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live