Ongezeko la mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limepelekea maelfu ya watu kutoweka.
Nigeria imeshuhudia mashambulizi ya umwagaji damu katika miaka ya hivi karibuni. Mashambulizi hayo yalianzia kwanza kaskazini na kisha kuenea katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa kundi la kigaidi la Boko Haram lilianzisha mashambulio na hujuma za mtutu wa bunduki mwaka 2009 kwa lengo la kujiimarisha kaskazini mwa Nigeria na kupanua mashambulizi yake hadi kwenye nchi za eneo la Ziwa Chad.
Isa Sanusi, Mkurugenzi wa Amnesty International na Wakfu wa Alamin nchini Nigeria ametangaza kuwa, katika kipindi cha miaka 14 iliyopita, zaidi ya watu 23,000 wametoweka kutokana na ongezeko la mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Mbali na Nigeria, kuanzia mwaka 2015 kundi la kigaidi la Boko Haram lilipanua wigo wa mashambulizi yake katika nchi zinazopakana na nchi hiyo ambazo ni Cameroon, Chad na Niger.../