Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanigeria walazimika kufunga kwa sababu ya bei ya juu ya vyakula

Wanigeria Walazimika Kufunga Kwa Sababu Ya Bei Ya Juu Ya Vyakula Wanigeria walazimika kufunga kwa sababu ya bei ya juu ya vyakula

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Raia kadhaa wa Nigeria katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno wanajinyima chakula baada ya gavana wao kutoa wito wa "kuingilia kati kwa Mungu" juu ya hali mbaya ya kiuchumi na usalama ya nchi.

Siku ya Ijumaa, Gavana Babagana Zulum aliwataka wakaazi kushiriki mfungo wa siku moja katika jimbo lote siku ya Jumatatu ili kukabiliana na kupanda kwa gharama ya chakula na misururu ya milipuko ya mabomu ya ardhini katika barabara zake kuu.

Bello Zabarmari, mkazi wa jimbo la Borno, aliambia BBC kwamba yeye na wengine wengi wanafunga na kumwomba Mungu kutatua matatizo yao.

"Tumeamka na mfungo leo na tunatumai maombi yetu yote yatajibiwa hivi karibuni, mkuu wa jimbo alifanya jambo sahihi kwa kuwaita watu kufunga," alisema.

Umar Shehu, mkazi anayefanya kazi na idara ya zima moto serikalini, alisema yeye na wenzake pia wanafunga kama alivyoagizwa na mkuu wa Jimbo.

Raia wa Nigeria wanapitia moja ya kipindi kigumu zaidi cha uchumi katika historia - bei ya vyakula na bidhaa muhimu imepanda katika miezi ya hivi karibuni.

Chanzo: Bbc