Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waniger waendelea kuandamana kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondoke

Wananchi Kituo Niger Waniger waendelea kuandamana kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondoke nchini mwao

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya raia wa Niger wamepiga kambi mbele ya kituo cha wanajeshi wa Ufaransa katika mji mkuu Niamey kutaka wanajeshi hao waondoke nchini mwao.

Tangu wiki iliyopita, wananchi wa Niger wamepiga kambi kwa kukusanyika mbele ya kituo cha wanajeshi wa Ufaransa mjini Niamey kupinga kuwepo kwa wanajeshi hao na kutaka waondoke nchini humo.

Katika siku ya sita ya mkusanyiko huo wa kuketi chini mbele ya kambi hiyo, mamia ya Waniger wamefunga mahema mbele ya kambi hiyo ya jeshi la Ufaransa kuonyesha azma thabiti waliyonayo ya kuendeleza harakati hiyo hadi askari hao wa kigeni waondoke katika ardhi ya nchi yao.

Wiki tano zilizopita, jeshi la Niger lilimuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Mohammed Bazoum na kuunda serikali ya kijeshi sambamba na kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondolewe nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live