Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wandani wa DP Ruto wasema BBI imelemaza uchumi wa taifa

96637c9926a0bc73 Wandani wa DP Ruto wasema BBI imelemaza uchumi wa taifa

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wakizungumza wakiwa kwa DP Ruto Karen, wanasiasa hao walisema Agenda Nne Kuu za Afya kwa Wote, Makazi Bora, Ukuaji wa Viwanda na Utoshelezo wa Chakula zimelemazwa kabisaWabunge hao walisema mara kwa mara wamekuwa wakiteta kuhusiana na jinsi Jubilee ilivyopuuza agenda zake ambazo iliahidi kuwatimizia wananchi wakati wa uchaguzi wa 2017Aidha waliongeza kuwa NASA imeharibu kabisa umoja uliokuwepo katika chama tawala cha Jubilee na isitoshe kuhakikisha muungao wa upinzani umevunjikaWandani wa Naibu Rais William Ruto wameshutumu Nasa na baadhi ya wabunge wa Jubilee kwa kuiteka serikali ya taifa kupitia BBI katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Katika taarifa yao ya Alhamisi, Agosti 5 baada ya mkutano wa Wabunge cha 'Hustlers' huko Karen, wanasiasa hao walisema kwa sababu hiyo, Agenda Nne Kuu za Afya kwa Wote, Makazi Bora, Ukuaji wa Viwanda na Utoshelezo wa Chakula

"La kusikitisha ni kwamba muungano wa Nasa, vinara wake na baadhi ya washirika wa Jubilee wameiteka nyara serikali na agenda zake zote kuu," mbunge wa Kandara Alice Wahome ambaye alisoma sehemu ya taarifa hiyo alisema.



Read also

David Murathe Aapa Raila Atakuwa Rais BBI Iwepo au Isiwepo

"Waliendesha vibaya uchumi na kusababisha kuongezeka kwa deni kwa kiasi kikubwa ambacho kimelifinya taifa."

Wabunge hao walisema mara kwa mara wamekuwa wakiteta kuhusiana na jinsi Jubilee ilivyopuuza agenda zake ambazo iliahidi kuwatimizia wananchi wakati wa uchaguzi wa 2017.

Wahome alisema NASA imeharibu kabisa umoja uliokuwepo katika chama tawala cha Jubilee na isitoshe kuhakikisha muungao wa upinzani umevunjika.

"Walilinyakua Bunge, walidhoofisha utawala wa sheria, walitishia uhuru wa Mahakama pasi na kutojali," alisema.

Wabunge hao walishutumu Nasa kwa kuendesha ukatili na unyama wa kibinadamu na pia uharibifu wa mali za kibinafsi katika maeneo kama Kariobangi, Ruai, kati ya mengine.

Pia waliwashutumu wenzao kwa kuhalalisha biashara zinazoendelea katika maeneo kama Nyamakima, Gikomba, Kamukunji, barabara ya Kirinyaga, barabara ya River kati ya zingine.

Aidha walidokeza kwamba kupitia mfumo Bottom Up Economy, watawawezesha Wakenya zaidi ya milioni 15 walio na kipato cha chini kuboresha maisha yao na kuongeza kwa idadi ya walipa ushuru hivyo basi kuimarisha uchumi wa taifa.



Read also

Ingia Jubilee Kama Unataka Kukosi Kiti 2022, Gavana Kiraitu Asema

Biashara kama hizo, walisema, zitajumuisha mama mboga, wachuuzi, wahudumu wa bodaboda, mafundi, wasanii kati ya wengine.

"Kwa sasa, tutaendelea kudhamini na kuunga mkono sheria na sera zinazozingatia watu ambazo zinaimarisha malengo ya mfumo wa chini wa uchumi na utawala." taarifa hiyo ilisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke